WiFi inaonyesha connected lakini internet haifanyi kazi

Jifunze hatua rahisi za kutatua tatizo la WiFi kuonyesha connected lakini internet haifungui kwenye simu au computer.

Kama WiFi inaonyesha connected lakini internet haifanyi kazi, tatizo linaweza kuwa kwenye router, simu, computer, DNS au provider wa internet.

Kwanza, restart router. Zima router kwa sekunde 30 kisha washa tena. Hii hutatua matatizo mengi ya connection.

Pili, jaribu kusahau WiFi kisha connect upya. Kwenye simu, nenda WiFi settings, chagua network yako, bonyeza Forget, kisha ingiza password tena.

Tatu, jaribu device nyingine. Kama device zote hazina internet, tatizo linaweza kuwa router au internet provider. Kama device moja tu ndiyo ina shida, tatizo lipo kwenye hiyo device.

Nne, angalia kama bundle au subscription ya internet imeisha.

Tano, kwenye Windows unaweza kutumia Network Troubleshooter au ku-run command hizi kwenye CMD kama administrator:

ipconfig /flushdns
ipconfig /release
ipconfig /renew

Mwisho, kama bado haifanyi kazi, wasiliana na internet provider wako.