Kama umebadili simu na unataka kurudisha WhatsApp chats zako, unatakiwa uwe na backup iliyohifadhiwa kabla.
Kwenye Android, WhatsApp hutumia Google Drive backup. Hakikisha simu mpya ina Gmail ile ile iliyokuwa kwenye simu ya zamani.
Install WhatsApp kwenye simu mpya, ingiza namba yako ile ile, kisha fuata hatua za verification. WhatsApp ikiuliza Restore Backup, bonyeza Restore.
Kwenye iPhone, WhatsApp hutumia iCloud backup. Hakikisha umeingia kwenye Apple ID ile ile iliyokuwa kwenye simu ya zamani.
Kama WhatsApp haioni backup, angalia mambo haya:
- Namba ya simu iwe ile ile
- Gmail au Apple ID iwe ile ile
- Internet iwe stable
- Backup iwe ilifanyika kweli kwenye simu ya zamani
Ni vizuri kuweka auto backup kila siku au kila wiki ili usipoteze messages zako.